Martin Saanya (Kulia) akikwepa kibano kutoka kwa wachezaji wa Simba katika mchezo wao na Yanga, Oktoba 1, mwaka huu
Taarifa iliyotolewa leo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kuwa suala la waamuzi hao limepelekwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili ishughulikie tatizo lao kitaalam.
Taarifa hiyo imedai kuwa maamuzi hayo yamefanyika baada ya kikao cha kamati ya usimamizi na uendeshaji ya bodi ya ligi, kuwaita na kuwahoji na kuangalia mkanda wa mchezo husika.
Imesema kuwa kamati hiyo imebaini mapungufu mengi ya kiutendaji yaliyofanywa na waamuzi hao, na hivyo kuitaka kamati ya waamuzi ishughulikie.