
Mcheza Tennis nambari mbili duniani Roger Federer amefuzu raundi ya 4 ya 16 bora katika michuano ya wazi ya Australia baada ya kumshinda Grigor Dimitrov kwa seti 3 kwa 1 katika mchezo wa raundi ya 3.
Federer ameshinda Dimitrov set 6-4, 3-6, 6-1, 6-4 na kufikisha ushindi wake wa 300 katika michezo yote ya Grand Slam aliyocheza.
Kwa upande wa wanawake, nyota namba moja duniani Serena Williams naye amefuzu hatua hiyo kwa kutumia dakika 45 kumuadhibu kinda katika mchezo huo mwenye umri wa miaka 18 raia wa Urusi Darya Kasatkina kwa seti 6-1 6-1.
Naye mchezaji namba moja kwa wanaume Novak Djokovic ambaye leo hakuwa katika ubora wake, amefanikiwa kupenya baada ya kumchapa Andreas Seppi kwa seti 3 kwa bila, 6-1 7-5 7-6.
Wengine waliofuzu 16 bora kwa wanawake na wanaume ni pamoja na Mrusi Maria Sharapova, Mswsi Belinda Bencic, Mjapani Kei Nishikori na Mfaransa Jo-Wilfried Tsonga