
Mwenyekiti wa kamati ya Ufundi ya Chama cha Mpira wa Wavu wa Ufukweni DAREVA Nassoro Sharifu amesema, mashindano hayo yamepangwa kufanyika kwa siku nne ili ili kujiandaa na Ligi ya mkoa na mashindano mengine ya kimataifa.
Sharifu amesema, klabu zote za Mkoa wa Dar es salaam zinatakiwa kushiriki ili kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa Ligi ya Mkoa ambayo itachezwa kwa muda mrefu ili kuwasaidia wachezaji kupata uzoefu wa kutosha.
Sharifu amesema, DAREVA imeandaa mashindano hayo ili kuzifanya klabu za mkoa huo kuwa na mashindano mengi kwa sababu mchezo huo mwaka jana ulipoteza nafasi ya kucheza mashindano ya kimataifa baada ya kushindwa kutamba katika michuano ya Afrika Mashariki na Kati yaliyofanyika jijini Dar es salaam.