Monday , 22nd Feb , 2016

Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal Mfaransa Asern Wenger amesema vijana wake wanapaswa kuhakikisha wanamnyamazisha Luis Suarez kama wanataka kuwafunga mabingwa watetezi wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya FC Barcelona hapo kesho.

Kocha wa Arsenal mfaransa Arsene(pichani) Wenger akizungumza na waandishi wa habari.

Akizungumza kuelekea mtanange huo kabambe utakaopigwa dimbani Emirate Wenger amesema licha ubora na kipaji walichonacho wachezaji Lionel Messi na Neymar Junior anaamini Suarez ni mchezaji hatari mwenye kujitolea hali inayowafanya kutengeneza muunganiko mzuri na wenzake.

Akitolea mfano Wenger amesema Suarez ameonesha kujitolea akiwa na timu ya taifa ya Uruguay akiwa na washambuliaji wenzake Diego Forlan na Edinson Cavani lakini pia uwezo aliouonesha akiwa Liverpool ni kielelezo tosha kuwa ni nyota wa kuchungwa uwanjani.

Mpaka sasa Suarez amefunga mabao 12 katika mechi 7 naye Messi akifunga mara 7 katika mechi 6 za mwisho na kuifanya Barcelona kuendeleza ubabe wa kucheza mechi 32 katika michuano yote pasipo kupoteza.