
Kikosi cha wachezaji wa Azam FC kikiwa katika mazoezi ya mwisho hapo jana Uwanja wa Dimani visiwani Zanzibar kabla ya kuvaana na Zimamoto Uwanja wa Amaan leo.
Mabingwa wa zamani wa michuano hiyo, Azam FC watacheza na Zimamoto kuanzia Saa 10:00 jioni, kabla ya mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga kumenyana na Jamhuri ya Pemba kuanzia Saa 2:30 usiku.
Mechi hizo zinafuatia mechi za ufunguzi za Kundi A zilizoanza Ijumaa Taifa Jang’ombe ikiilaza 1-0 Jang’ombe Boys.
katika mechi za jana wenyeji KVZ walianza vibaya baada ya kufungwa 2-0 na mabingwa watetezi, URA wakati vinara wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Simba wakiichapa 2-1 Taifa Jang'ombe.
Kwa sasa Simba inashika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi B ikiwa nyuma ya URA , lakini timu zote tatu yaani Simba, Taifa Jang'ombe na URA zina point 3 kila moja
Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu Mzambia, George Lwandamina imepania kufanya vizuri kwenye michuano ya mwaka huu baada ya kutokuwa na matokeo mazuri kwa miaka minne iliyopita.