
Heritier Makambo
Dismas amesema mchezaji huyo yupo nchini kwao DR Congo kwa mapumziko maalum na hivi karibuni atarejea nchini.
''Makambo ni mchezaji wa Yanga alisafiri kwenda kwao na hawezi kuondoka kihuni kwasababu ana mkataba na ni mchezaji wa kimataifa kwahiyo atarudi tu, muda mwingine masuala ya mawasiliano yanaweza kuwa sawa au yasiwe sawa'', amesema.
Mapema leo taarifa zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mshambuliaji huyo ametoweka kambini na mabegi yake na hajulikani alipo.
Yanga ambayo inaongoza ligi ikiwa na alama 50, kesho inashuka dimbani kucheza dhidi ya Mwadui FC kwenye mchezo wake wa 19 kwenye ligi kuu soka Tanzania bara.