
Mashabiki wa Yanga wakiongozwa na mhe. Dr. Mwigulu Nchemba kufurahi
Kampeni hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa michezo nchini pamoja na viongozi wa serikali wakiongozwa na Waizri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alialikwa kama mgeni rasmi.
Mgeni rasmi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahidi kutoa kiasi cha Sh. 10 milioni huku pia akisema kuwa ameagizwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz awatangazie wanachama wa Yanaga kuwa atachangia kiasi cha Sh. 200 milioni ambayo ataikabidhi pindi atakaporejea Tanzania kutokea nchini Marekani.
Kampuni ya GSM imetoa ahadi ya Sh. 300 milioni kuichangia klabu hiyo, huku Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akiahidi kuchangia kiasi cha Sh. 5 milioni.
Kamati ya kumasisha uchangiaji wa klabu hiyo inayoongozwa na Naibu Waziri, Anthony Mavunde, imeahidi kutoa kiasi cha Sh. 50 milioni sambamba na safu ya uongozi wa klabu hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti wa klabu, Dr. Mshindo Msolla ambayo imeahidi kuchangia Sh. 50 millioni.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, mhe. Paul Makonda, ameahidi kuwapatia uwanja eneo la Kigamboni Jijini Dar es salaam ambao watautumia kujenga kiwanja chao, akisema kuwa ni kwa ajili ya kulipa deni la Rais mstaafu Jakaya Kikwete ambaye aliwahi kuchangia Sh. 30 milioni kwa ajili ya uwanja wa klabu ya Simba uliopo Bunju.
Kwnye halfa hiyo pia wametambulishwa wachezaji wapya wawili, Juma Balinya ambaye aliibuka mfungaji bora wa ligi kuu nchini Uganda msimu uliopita, pamoja na Abdulaziz Makame.