Tuesday , 21st Mar , 2017

Mabingwa wa Tanzania, Yanga SC imepangwa kukutana na timu ya MC Alger ya Algeria katika hatua ya pili ya 16 bora ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kusaka nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya michuano.

Hiyo ni kwa mujibu wa matokeo ya droo iliyochezeshwa leo na shirikisho hilo, iliyohusisha timu 16 zilizofuzu kutoka hatua ya kwanza ya 16 bora ya michuano hiyo, na timu nyingine 16 zilizoondolewa katika raundi ya pili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika ikiwemo Yanga.

Katika michuano ya Klabu Bingwa, Yanga ilitolewa na Zanaco ya Zambia kwa bao la ugenini baada ya kufungana bao 1-1 nyumbani, na kisha kutoka suluhu ugenini nchini Zambia.

Katika raundi hii, zinasakwa timu 16 zitakazoingia kwenye hatua ya makundi, na mechi zitapigwa kati ya Aprili 7-9 na kurudiana ni kati ya April 14-16 mwaka huu.

Matokeo kamili ya droo yako hivi.................