Hayo amethibitisha na taarifa zilizotolewa na Afisa Habari wa timu hiyo Dismas Ten wakati alipokuwa anazungumza na mwandishi wa habari hii ya kutaka kujua sababu kubwa ya wao kuzuiliwa.
"Ni kweli tumezuiliwa kufanya mazoezi asubuhi ya leo kama nilivyotoa taarifa katika ukurasa wetu wa timu na meneja wa uwanja Nsajigwa Gordon ambapo ametuambia ule sio uwanja wa mazoezi ila upo kwa ajili ya mechi", amesema Dismas.
Timu ya Yanga inatarajia kushuka dimbani siku ya Jumamosi (Februari 10, 2018) kuvaana St. Louis inayotokea visiwa vya sheli sheli na katika mashindano ya kimataifa.



