
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa klabu hiyo Jerry Muro kwa niaba ya uongozi mzima wa Yanga, imesema uongozi unathamini juhudi za wachezaji hadi kupata mabao hayo mawili kwa bila, kwenye mchezo huo.
Taarifa hiyo imesema uongozi utaenzi jitihada hizo kwa kuwa ni mafanikio ya klabu na wanachama wa klabu hiyo wanatakiwa kujua thamani ya wachezaji kutoka kwa uongozi huo.
Aidha kwa upande mwingine,kikosi cha Yanga kimeanza mazoezi hii leo kwenye uwanja wa chuo cha polisi kurasini jijini Dar es Salaam na kesho kikosi hicho kitaingia kambini rasmi kujiandaa na mchezo wa kombe la FA dhidi ya JKT Mlale Jumatano Februari 24 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.