Saturday , 1st Dec , 2018

Uongozi wa vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara, Yanga umetangaza majina ya wajumbe wapya wa kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo ambao watafanya kazi sambamba na kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Makao makuu ya Yanga

Wajumbe hao wa kamati wametangazwa leo na mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga, Siza Lyimo ambapo amebainisha kuwa hayo ni makubaliano ya kikao cha Novemba 16 mwaka huu kati ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Kamati ya Utendaji ya Yanga.

Mbali na hilo Lyimo ametangaza kuwa, Samwel Lukumay ameteuliwa kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga wakati yeye (Siza Lymo) akiteuliwa kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti.

Amesema uamzi huo wa wao kuteuliwa ni kuhakikisha shughuli zote za klabu zinaendelea chini ya usimamizi madhubuti.

Kamati hizo mbili za uchaguzi hii ya Yanga na ile ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ndio zitakazo fanikisha uchaguzi mkuu wa Yanga Januari 13, 2019.

Wajumbe hao ni:-
1. Jabir Katundu.
2. Daniel Mlelwa.
3. Samwel Mapande.
4. Mustafa Nagari.
5. Wakili Godfrey Mapunda.
6. Edward Mwakingwe.
7. Samuel Mangesho.