
Kocha Fadlu Davids yeye ndiye sababu ya timu yake kuongoza msimamo wa ligi msimu huu licha ya kuwa ndio msimu wake wa kwanza kwenye kikosi hiko huku kukiwa na presha kubwa ya kuhitaji kushinda ubingwa wa ligi sambamba na kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika kwa ngazi za Vilabu. Kocha huyo raia wa Afrika ya kusini ameijenga timu yake kupata matokeo chanya katika hali yoyote bila kuangalia inachezaje.

Timu chache ndani ya hii miaka mitano ya hivi karibuni zimeweza kuwa na muendelezo mzuri wa kushiriki michuano ya Afrika na kufika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo kama Simba SC.

Yanga SC imeshinda michezo miwili mtawalia ya ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya kwanza tangu ipoteze dhidi ya kikosi cha Tabora United kutokea mkoani Tabora.

Ubora huu wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Fadlu Davies unatokana na upana wa kikosio hiko na ubora wa Mchezaji mmojammoja ulioongezeka kwenye kikosi hiko.

Diarra atakosa michezo ya ligi kuu kuu Tanzania bara pamoja na ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe Januari 3, Al Hilal januari 10, na MC Algers utakaochezwa Januari 17 2025 uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Klabu ya Tanzania Prisons kutoka Mkoani Mbeya imeachana na Kocha Mkuu Mbwana Makata pamoja na Msaidiz wake Renatus Shija kutokana na mwenendo mbovu wa matokeo.

Magoli ya Simba SC yamefungwa na Leonel Ateba Mbida aliyefunga dakika ya 35 na 45 kipindi cha kwanza magoli hayo Ateba amefikisha magoli 5 katika ligi kuu Tanzania bara akionekana kuendelea kuimarika kadri siku zinavyozidi kwenda akiwa na kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Sead Ramovic raia wa Ujerumani imeshinda mchezo mmoja tu dhidi ya Namungo FC ikipoteza dhidi ya Azam FC, Tabora United,Al Hilal,MC Algers na kutoka sare dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa makundi wa ligi ya mabingwa Afrika.

Mfungaji bora huyo wa mashindano ya kombe la Dunia la mwaka 2002 atashindana na Rais wa sasa wa CBF Ednaldo Rodrigues katika uchaguzi mkuu utakaofanyika 2026.

Lookman amewashinda Achraf Hakimi wa PSG na timu ya taifa ya Morocco,Serhou Guirassy wa Borrusia Dortmund na timu ya taifa ya Guinea na Ronwen Williams wa Afrika ya Kusini.

Klabu ya Simba inashida ya uwepo wa Mchezaji anayeweza kucheza kwa kutokea pembeni ambaye anaweza kufunga na kutengeneza magoli.Viungo wa pembeni wa timu ya Simba wanachangamoto ya kutengeneza nafasi Kibu Denis,Radack Chasambi,Edwin Balua,Joshua Mutale wote mchango wao wa kufunga na kutengeneza nafasi umekuwa mdogo msimu huu.

Simba SC yenyewe itaingia uwanjani siku ya Jumamosi ikiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya FC Bravos ya kutokea Angola kwenye mchezo wa kwanza wa makundi uliochezwa uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es salaam.

Kakiongoza kikosi cha Mashetani Wekundu la Jiji la Manchester kushinda michezo mitatu na kutoka sare mchezo mmoja wa ligi dhidi ya Chelsea mchezo uliopigwa dimba la Old Trafford aliamua kuondoka baada ya kuambiwa hatokuwa sehemu ya benchi la ufundi la Kocha mpya wa timu hiyo Mreno Ruben Amorim.

Kipigo hiko kutoka kwa Liverpool kwenye uwanja wa Anfield kumeifanya Madrid kusalia na alama zake 6 baada ya kucheza michezo mitano inashika nafasi ya 24 katika mashindano yenye timu 36. Kikosi cha Los Blancos ndio mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa barani msimu huu inakutana na wakati mgumu kutokana na kutokuwa kwenye kiwango chake kilichozoeleka katika mashindano ya msimu huu wenye mfumo tofauti na uliozoeleka

Kipigo hiko kutoka kwa Liverpool kwenye uwanja wa Anfield kumeifanya Madrid kusalia na alama zake 6 baada ya kucheza michezo mitano inashika nafasi ya 24 katika mashindano yenye timu 36. Kikosi cha Los Blancos ndio mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa barani msimu huu inakutana na wakati mgumu kutokana na kutokuwa kwenye kiwango chake kilichozoeleka katika mashindano ya msimu huu wenye mfumo tofauti na uliozoeleka