Wednesday , 9th Sep , 2015

Star wa muziki wa dansi Taarsisi Masela Joto ambaye hivi sasa ameachia wimbo wake mpya unaoitwa 'Usingizi' amesema kuwa hii ni mara yake ya kwanza kutengeneza wimbo kwa kutumia dakika tatu tu tofauti na nyimbo nyingi za dansi kuwa ndefu mno.

Star wa bendi ya muziki wa dansi Akudo Impact Taarsisi Masela Joto

Star huyo ambaye anaimbia bendi maarufu ya Akudo Impact amesema kuwa yeye bado yupo ndani ya bendi hiyo licha ya kufanya muziki wake nje ya kundi, akielezea kuwa lengo la kuimba wimbo huo kwa kutumia dakika tatu ni kutokana na muziki wao wa dansi kutopigwa sana katika Club za Disco.