Tuesday , 15th Sep , 2015

Baada Azam FC kuichapa Tanzania Prisons 2-1 katika pazia la ufunguzi wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara siku ya Jumamosi, kocha mkuu Muingereza Stewart Hall amesema, kipigo hicho ni mwanzo tu na mpango wake ni kuchapa timu zote zinazokuja mbele yetu.

Kocha Stewart amesema, anataka timu ishinde kwa mabao mengi kutokana na ubora wa wachezaji alionao hasa kwenye safu ya ushambuliaji ambao ni Mrundi Didier Kavumbagu, Mkenya Allan Wanga, Mu-Ivory Coast Kipre Tchetche, Ame Ally, Bocco, Mcha Hamis, Ramadhani Singano 'Messi' na Farid Mussa lakini wanamwangusha.

Azam FC inayoshikilia nafasi ya pili ikitanguliwa na Yanga kwa goli moja imeondoka jana kuelekea mjini Shinyanga kujiandaa na mchezo dhidi ya Stand United hapo kesho uwanja wa Kambarage.