
Nkurunzinza ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na ujumbe wa mabalozi kutoka umoja wa mataifa ambao wapo nchini Burundi kwa lengo la kutaka kuleta amani ya kudumu baada ya kutokea mapigano,vifo,wakimbizi na machafuko baada ya uchaguzi uliomrejesha madarakani Rais Nkurunzinza.
Pia Rais Nkurunzinza amekataa wito wa kufufuliwa kwa juhudi za upatanishi na kupelekwa kwa kikosi cha wanajeshi 5,000 wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika nchini humo ili kurejesha uthabiti.
Hata hivyo Umoja wa Afrika utafanya mkutano wa kilele kati ya tarehe 30 na 31 mwezi huu wa Januari na mzozo huo wa Burundi ukitarajiwa kupewa kipaumbele katika mazungumzo ya mkutano huo.
Chanzo VOA
