
Watu wenye ulemavu nchini wametakiwa kusimamia haki zao ya kuthaminiwa katika jamii kwa kuhakikisha kuwa kamwe jamii haitumii mapungufu ya hali ya ulemavu waliyonayo kama sababu ya kuwanyanyasa na kuwabagua.
Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi, ametoa wito huo jijini Dar es salaam leo wakati wa hafla ya chakula cha mchana alichowaandalia watu wenye ulemavu nchini, ambapo amesema watu wenye ulemavu wanastahili haki zote na heshima kama ilivyo kwa watu wengine kwenye jamii.
Hata hivyo Dkt. Mengi ameiomba jamii kudumisha moyo wa upendo, hasa kwa walionacho kuwajali fukara na watu wasio na kipato, kwani kwa kufanya hivyo itasadia kujenga jamii inayojali na kuwa na huruma kwa watu wenye mahitaji.