Wednesday , 24th Feb , 2016

Muandaaji wa muziki wa kizazi kipya nchini (Director) Hanscana amemshangaa msanii Q Chief kwa kauli yake kwamba kwa upande wa Tanzania hakuna muandaaji mwenye uwezo wa kutengeneza kazi yake kwa sasa .

Hanscana amesema kwamba msanii huyo hawezi jilinganisha naye maana kizazi chake ni cha zamani na yeye hawezi kufanya naye kazi kwa sababu muda wake umekwisha.

''Q Chief sasa hivi yeye ni sawa na kibanda hivyo hawezi kujifananisha na ghorofa,mimi siwezi fanya kazi na yeye nafanya kazi za kueleweka na watu wa kizazi cha sasa na sii yeye''Amesema Hanscana

Muandaaji huyo ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha E NEWS kinachorushwa na kituo cha EATV.

Wiki iliyopita msanii Q Chief alisema kwamba yeye hawezi kutengenezea video ya kazi zake hapa nchini tena maana hapa nchini waandaaji wa muziki hawana viwango vizuri vya video bali hutaka fedha nyingi.