
Meneja wa Simba Abbas Gazza amesema kikosi hicho kinaweka kambi visiwani humo kikiwa na lengo la kuendelea kuwania Ubingwa w ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.
Gazza amesema, kikosi hicho kitarejea Dar es Salaam Jumamosi tayari kabisa kwa mechi hiyo itakayopigwa Jumapili Uwanja wa Taifa.
Gazza amesema, mchezo uliopita kulikuwa na mapungufu makubwa yaliyochangia kushindwa kupata pointi tatu dhidi ya Azam FC baada ya kutoa suluhu ya bila kufungana hivyo anaimani katika mchezo unaofuata wataweza kupata pointi tatu ambazo zitaweza kuwaweka katika nafasi nzuri za kuweza kufukuzia ubingwa wa Ligi ambao mpaka sasa Yanga ndiye anayeongoza kwa kuwa na pointi 68.
Kwa upande mwingine Gazza amesema Kiungo wa Simba, Ibrahim Ajib amejiunga na kikosi cha Simba na kuanza mazoezi rasmi.