Friday , 6th May , 2016

Winga wa kimataifa wa Tanzania Farid Mussa Malik wa klabu ya Azam FC amefaulu majaribio katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania.

Winga wa Kimataifa wa Tanzania Farid Mussa Malik

Tenerife sasa inatarajiwa kuingia katika mazungumzo na Azam FC juu ya kumnunua mchezaji huyo ingawa wazo lao la awali ni kumchukua kwa mkopo wa miaka miwili.

Kwa upande wake, Farid amesema amefurahia matokeo hayo kwani haikuwa kazi nyepesi kwake kuweza kuwaridhisha maofisa wa benchi la ufundi la Tenerife kutokana na mpira wa Ulaya kuwa mgumu.

Awali, Farid ilikuwa apelekwe moja ya klabu za Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga, kati ya Las Palmas na Athletic ya Bilbao kwa majaribio, lakini wakala wake akashauri mchezaji huyo aanzie timu ya Daraja la Kwanza Hispania ili kupata nafasi ya kucheza na kuinuka haraka.