Friday , 22nd Jul , 2016

Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi imesema wiki ijayo itatangaza hadharani majina ya waajiriwa ambao wanadaiwa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu,mkopo walikopeshwa wakati wakisoma katika vyuo vya elimu ya juu.

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imesema wiki ijayo itatangaza hadharani majina ya waajiriwa ambao wanadaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, mkopo walikopeshwa wakati wakisoma katika vyuo vya elimu ya juu.

Hayo yamebainika leo jijini Dar es salaam wakati Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Maimuna Tarishi akifunga maonesho ya 11 ya vyuo vya elimu ya juu nchini yaliyoshirikisha vyuo kutoka ndani na nje ya nchi.

Hatua hiyo inakuja baada ya serikali kuwataka wanufaika hao kuanza kurejesha fedha hizo kwa hiari kushindikana ili kuwanufaisha wengine vinginevyo majina hadharani ya wadaiwa hao.

Kwa upande mwingne, ubora wa elimu unaotolewa na vyuo hivyo nao umeonekana kuporomoka na hivyo kuathiri ushindani wa wanafunzi kujiunga na vyuo hivyo, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Maimuna Tarishi anaitaka Tume ya Vyuo Vikuu nchini TCU na Baraza la Elimu ya Ufundi nchini NACTE kuzingatia vigezo wakati wa udahili.

Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU, Eliuta Mwageni amesema wanaendelea kushughulikia changamoto za udahili zilizopo ili kukabiliana na udanganyifu kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya elimu ya juu.

Serikali imetaka vyuo hivyo kujikita kufundisha fani za sayansi, uhandisi na elimu ya teknolojia ya habari na mawasiliano, hali inayoitikiwa na vyuo vilivyoshiriki maonesho hayo ikiwa ni pamoja na Pendo Mganga ambaye ni mhadhiri wa Jordan University pamoja na Eastern Mediteranian University cha nchini Uturuki.