Tuesday , 6th Dec , 2016

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amesema anataka kupunguza matumizi ya serikali yake kwa kufuta zabuni ya kuagiza ndege mpya za kumsafirisha Rais wa Marekani maarufu kama Air Force One.

Air Force One - Ndege zinazotumiwa na Rais wa Marekani

 

Katika ukurasa wake wa Twitter, Bw. Trump ameandika kuwa kampuni ya Boeing inatengeneza ndege mpya za Air Force One aina ya Boeing 747 kwa ajili ya Rais na kusema kuwa gharama yake ya dola bilioni nne ni kubwa mno.

Jeshi la Anga la nchi hiyo limesisitiza ndege hizo ziharakishwe kwani zile za sasa zimechoka na imekuwa gharama kubwa kuzifanyia matengenezo.

Hata hivyo, Bw. Trump hatatumia ndege hizo mpya npaka mwaka 2020 endapo atashinda muhula wa pili wa uongozi .

Donald Trump

Kwa sasa Rais huyo mteule anatumia ndege yake binafsi ya Boeing 747, lakini atapaswa kutumia Air Force One ambayo ina vifaa vya kisasa vya usalama, ulinzi na mawasiliano.