Saturday , 17th Dec , 2016

Msanii Tunda Man ametoa maelezo juu ya wimbo wake wa debe tupu, ambao umeibua gumzo kubwa kwa sasa kwa mashabiki wa muziki na kusema kuna msanii kamuimba, baada ya kutoa picha ya cover la wimbo huo.

Picha ya cover ya wimbo wa debe tupu wa msanii Tunda man ulioleta gumzo mtaani.

Akizungumza na East Africa Television, Tunda Man amesema wimbo huo hajamuimba mtu yeyote, isipokuwa ni kwa watu wote wenye tabia za debe tupu.

Pia msanii huyo amezungumzia mipango yake ya kuachia ngoma za Tip Top bila kuruhusiwa na uongozi, akidai kuwa iwapo wataendelea kusubiri uongozi itawaathiri wao.

Mtazame hapa chini akizungumzia hilo na mpango wake wa kuachia ngoma za Tip Top bila kuruhusiwa na uongozi.