
South gate katika mazoezi ya England
Uingereza imesafiri hadi Ujerumani kuivaa timu ya Taifa ya nchi hiyo, kwenye mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA, utakaopigwa kwenye dimba la Signal Iduna Park, Dortmund, majira ya saa 4 na dakika 45 usiku huu.
Southgate amesema mipango ya Uingereza kuendeleza soka lake ipo kwenye mstari, baada ya kufanya mageuzi kwenye soka la vijana kwa kuanzishwa academy nyingi na kuandaa kozi za makocha.
Ujerumani inasifika kuwa na mfumo mzuri wa soka la vijana uliojengwa kuanzia mwaka 2003, na matunda yake ni kizazi cha kina Mesut Ozil (Arsenal), Tony Kloose (Real Madrid), Thomas Müller (Bayern Munich) na wengineo wengi, waliokuja kuipa Ujerumani kombe la dunia, mwaka 2014 nchini Brazil.