Kutokana ushindi huo Warriors wanafikisha jumla ya michezo sita bila ya kupoteza tangu kuanza mfululizo wa michezo ya nusu fainali ya ukanda wa magharibi huku ukiwa ni mchezo wa 13 mfululizo bila kupoteza.
Timu hizo zitakutana tena siku ya Jumapili hii katika kucheza mchezo wa pili wa fainali ya ligi kuu nchini marekani NBA katika uwanja wake wa nyumbani Oracle Arena.
Warriors walipata nafasi ya kuingia nusu fainali baada ya kuichapa San Antonio Spurs kwa point 129-115 mchezo ulipigwa mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu.



