
Mo Music amefunguka hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya siku ya jana Timbulo kudai kuwa yeye ndiyo amemsaidia Mo Music kwa kiasi kikubwa katika muziki pamoja na kumshauri mambo mengi ikiwa na usimamizi wa kazi zao za muziki.
"Kukaa kwangu kimya kisanaa kusimfanye Timbulo afikiri kuwa nimekufa kwa kuwa sehemu niliyopo inanitosheleza na ndiyo maana hata Timbulo aliwahi kuniomba nifanye naye kolabo ya wimbo ambao nilimkatalia na baadaye alienda kufanya na Baraka The Prince", amesema Mo Music.
Kwa upande mwingine Mo Music amesema endapo hata ikitokea wakandaa tamasha la bure kati yake na Timbulo amedai kuwa hatoweza kumzidi kwa chochote.