Thursday , 10th Aug , 2017

Baraza la Michezo Taifa (BMT)  hii leo wametangaza rasmi uchaguzi mkuu wa chama cha mchezo wa netball ambao utafanyika tarehe 30 mwezi 9 mwaka huu.

Makamu Mwenyekiti wa Chaneta mama Zainabu Mbiro amesema uongozi uliopo madarakani ambao ulichaguliwa mwaka 2013 uko tayari kuachia madaraka na kukabidhi kijiti kwa uongozi mwingine huku akipongeza mikoa 15 ambayo tayari imefanya uchaguzi huku chama hicho kikiwa na wanachama katika mikoa 26 na kuwasihi wengine wamalizie uchaguzi ili waweze kushiriki uchaguzi wa kitaifa

Msemaji wa BMT Najah Bakari amesema nafasi zinazogombea ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Mkuu Msaidizi na Mweka hazina ambapo fomu za ushiriki zinatajwa kugharimu shilingi laki 1.

Hata hivyo katika nafasi 6 za wagombea wa kuchaguliwa, mgombea anayetaka kugombea atalipa ada ya fomu elfu 50