
Viongozi wanaoshitakiwa ni Msimamizi wa ligi kuu kituo cha Mtwara Dunstan Mkundi, Katibu wa chama cha soka Mtwara Kizito Mbano, Muhasibu msaidizi wa Simba SC Suleimani Kahumbu na Katibu msaidizi wa klabu ya Ndanda FC Selemani Kachele.
Viongozi hao wameshitakiwa kwa kugushi na udanganyifu wa mapato ya mlangoni kwenye mchezo wa ligi kuu namba 94, uliozikutanisha Ndanda FC na Simba SC Disemba 30 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Sekretarieti hiyo imewashitaki viongozi hao kwenye Kamati ya Maadili ambayo itaketi Januari 18 mwaka huu. Katika mchezo huo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 mabao ambayo yalifungwa na mshambuliaji John Bocco.
Aidha Kamati hiyo ya maadili inaongozwa na Mwenyekiti Wakili Hamidu Mbwezeleni, makamu Mwenyekiti Steven Zangira na Wajumbe ni Glorious Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhresa.