Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo (Jumapili) na kudai kutakuwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa ambazo zinatarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Mara, Simiyu, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Morogoro, Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na visiwa vya unguja na Pemba.
Mbali na hilo, TMA imesema kutakuwepo upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2 ambavyo vinatarajiwa katika ukanda wote wa Pwani
Kwa taarifa kamili angalia hapa chini






