Thursday , 29th Nov , 2018

Baada ya beki mpya wa Simba, Zana Coulibaly kutua nchini jana na kufanikiwa kutazama mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika kati ya timu yake mpya ya Simba dhidi ya Mbabane Swallows, ameweka wazi kuwa kiwango cha Simba ni kikubwa.

Mashabiki wa Simba na Zana Coulibaly

Kupitia mwenyeji wake ambaye ni mmoja wa viongozi wa kamati ya usajili ya klabu hiyo, jana jioni baada ya mchezo alisema Zana ameona mchezo na amekiri kuwa Simba ina wachezaji wenye kiwango kikubwa.

''Pamoja na uchovu wa safari lakini hakutaka kukosa mchezo, ameitazama timu na kusema wachezaji ni washindani na wana vipaji vikubwa ila hatajataka kuongea sana kwasababu bado hajawa mchezaji wetu kamili'', alieleza.

Zana Coulibaly leo anatarajiwa kusaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo ambayo imemleta mahsusi kuziba pengo la Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi.

Mlinzi huyo wa kulia alikuwa mchezaji wa timu ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast ambayo ilikuwa kundi moja na Simba kwenye ligi ya mabingwa Afrika msimu wa 2002/2003.