
Moja ya picha ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta
Watuhumiwa hao ambao ni Kennedy Ochieng, mwenye umri wa miaka 22 na Bw Kevin Ogega, mwenye umri wa miaka 25, ambao wote ni wanafanyakazi wa kampuni ya kubeba mizigo katika uwanja huo, wamedaiwa kuiba pesa za abiria baada ya kukutwa nazo kufuatia msako mkali.
Licha ya kupatikana kwa pesa hizo, Polisi nchini Kenya haijathibitisha ni wapi pesa hizo zimepatikana.
Matukio ya abiria kuibiwa pesa katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) yamekuwa yakiripotiwa mara kadhaa, ambapo mwezi Mei mwaka huu raia mmoja wa Iran aliyetambulika kwa jina la Mehrah Hassan ,30, aliripoti polisi kufuatia kuibiwa kiasi cha Dola za kimarekani 7,500 katika begi yake akiwasiri katika uwanja huo akitokea nchini Qatar.