
Wachezaji wa Simba kwenye mazoezi
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa 12 kwa Simba msimu huu, ulichezwa Ijumaa ambapo zilikuwa zimebaki siku kadhaa tu kabla ya Simba kucheza mchezo wake wa hatua ya awali ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows.
Baada ya mechi hiyo kuisha kwa suluhu, kocha wa Simba Patrick Aussems alisema sababu kubwa ya matokeo hayo ni wachezaji wake kufikiria zaidi mchezo wa kimataifa dhidi ya Mbabane Swallows, kitu ambacho kinazua hofu kuwa katika mchezo wa leo dhidi ya KMC hakitajirudia?
Kwa upande wa msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara alisema kuwa wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa wanaiheshimu KMC kutokana na kuwa miongoni mwa timu zenye vijana wenye vipaji vikubwa.
Hata hivyo wachezaji wa Simba leo watacheza kwa tahadhari kubwa wakiwa wanawaza mchezo wa Jumapili dhidi ya Nkana FC ambapo tayari wapinzani wao hao wapo nchini na leo watakuwa uwanja wa taifa kutazama mchezo huo unaoanza saa 12:00 jioni.