
Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika, TLS, Fatma Karume.
Fatma Karume ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na www.eatv.tv ambapo alijibu swali juu ya kuonekana kwake kwenye kikao cha vyama 6 vya siasa vya upinzani nchini mkutano ambao ulifanyika Zanzibar na kutoa maazimio mbalimbali.
"Mimi nilialikwa na vyama vya upinzani kuwapa mafunzo juu ya Katiba yetu, ili waelewe wanachokijadili kuhusu katiba yetu, lakini pia nikialikwa na CCM kuwaeleza kuhusu Katiba nitawaeleza kila mwanasiasa akitaka kujua katiba yetu tutaishi maisha bora zaidi."
"Kwa hiyo mimi chama chochote kikiniita kiwe CCM, CUF, CHADEMA, ACT -Wazalendo wakiniita kuwaeleza kuhusu Katiba yetu nitaenda kwa sababu ni wajibu wangu," amesema Fatma Karume
Aidha Fatma Karume amesema "CCM hawaniiti kujifunza kuhusu katiba yetu ila wakinialika nitaenda, niko tayari kwenda hata kesho nitaenda na waelewe na msimamo wangu kwenye mafunzo huwa hautabadilika."