Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Bilionea Jack Ma aondoka Alibaba

Wednesday , 11th Sep , 2019

Bilionea kutoka China na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Alibaba, Jack Ma, ametangaza kustaafu majukumu yake kwenye kampuni ya Alibaba ambayo alianzisha yeye na wenzake 18 miaka 20 iliyopita.

Jack Ma

Jack Ma amestaafu nafasi hiyo baada ya kutimiza umri wa miaka 55 na sababu kubwa iliyomfanya kuachia ngazi anasema ni kuruhusu uwezo wa vijana kujionesha kwa kuiongoza kampuni hiyo kwa sababu anaamini amewafundisha mengi hivyo anataka kuona uwezo wao wa kuisogeza Kampuni hiyo inayotajwa kuingiza kipato kikubwa Duniani.

Kampuni ya Alibaba ilianzishwa miaka 20 iliyopita kwa mtaji wa Tsh.Milioni 138 lakini kwa sasa ina thamani ya Tsh. Trilioni 966 huku Jack Ma akitajwa kuwa na utajiri wa Tsh. Trilioni 92. 
Kabla ya kuanza biashara Jack Ma amewahi kuwa Mwalimu na amesema anataka kurudi tena kufundisha pia kuhakikisha anatoa misaada ya kutosha kwaajili ya kusaidia jamii.

Jack Ma anasema anategemea kuona Kampuni hiyo ikiendelea kufanya uwekezaji mkubwa kwaajili ya kusaidia jamii pia kuhakikisha ina boresha masuala ya teknolojia kama mapinduzi ya 5G pamoja na akili bandia (Artificial Intelligence).

"Sio rahisi kuwa na Kampuni yenye nguvu lakini ni ngumu zaidi kuwa na Kampuni nzuri,” alisema.

"Kampuni yenye nguvu hutajwa kutokana na uwezo wake wa kiuchumi lakini Kampuni nzuri ni ile inayowajibika na yenye ustaarabu,” aliongeza zaidi.

Alibaba ni Kampuni inayojishughulisha na biashara mbalimbali kama masuala ya kiteknolojia, biashara mtandaoni, utengenezaji wa vifaa mbalimbali vya teknolojia na uwekezaji.

HABARI ZAIDI

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90