Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema
Akizungumza leo Oktoba 12, 2019 na EATV & EA Radio Digital, Lema amesema kuwa ameamua kutoa ofa hiyo baada ya kuona magari yanayofanya shughuli hiyo kuwa ni machache na kwamba yupo tayari yawekwe bendera za Chama cha Mapinduzi (CCM).
''Nimewaomba niwape ofa ya magari matano mpaka kumi, watangazie wananchi kwenda kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa, wananchi hawajui na gari ni chache, kwahiyo kama wanahisi kutangazia huko kunaweza kukasababisha wafuasi wengi wa CHADEMA, wakapata 'awareness' nimewaomba hayo magari yawekwe bendera za CCM lakini niyalipie mimi'' amesema Lema.
Hatua hii ya Lema kutoa ofa hiyo ni baada ya yeye kupokea barua kutoka kwa Mkuu wa Polisi Wilaya, iliyomzuia kufanya mikutano yake ya hadhara jimboni kwake, ambapo hapo siku ya jana Oktoba 11, 2019, aliruhusiwa kuendelea na mikutano yake kama kawaida.