Wednesday , 11th Dec , 2019

Mchambuzi wa michezo kutoka East Africa Television na East Africa Radio Tigana Lukinja ambaye ni kocha wa soka, ameondoka nchini leo Desemba 11, 2019 kwenda nchini Ghana kwaajili ya mradi maalum wa kusaka vipaji vya soka, unaoratibiwa na Bundesliga.

Mchambuzi wa michezo Tigana Lukinja.

Tigana ameeleza kuwa wakiwa Ghana yeye na wenzake watasaka vipaji vya umri wa miaka 13-17 kwa Wasichana na Wavulana, kwa ajili ya Academy za Ujerumani.

'Kuna kitu Bundesliga wamekianzisha kwa ukanda wa Africa wanakiita 'Bundesliga Football School' ambapo mimi nimejumuishwa kwenye timu ya ufundi kusaka hivi vipaji vitakavyokwenda kupikwa kwenye Academy mbalimbali za soka nchini Ujerumani', amesema Tigana wakati anaondoka.

Aidha amebainisha faida za mradi huo kwa kusema, 'faida ni kubwa sana, ikiwemo mimi binafsi kuongeza ujuzi kwenye eneo la 'scouting' kimataifa, na baadaye nitaomba mradi huu ufanyike kwetu Tanzania'.