Wednesday , 11th Dec , 2019

Afisa Nyama kutoka Bodi ya Nyama Tanzania, Edgar Mamboi, amewataka wananchi kufuata taratibu pindi wanapotaka kuwachinja wanyama mbalimbali, ili kujiweka kwenye mazingira salama wakati wa kula kitoweo chochote.

Supu

Mamboi ametoa kauli hiyo leo Desemba 11, 2019, wakati akizungumza kwenye Kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 asubuhi, ambapo amesema kuna idadi kubwa ya watu hawafuati taratibu za kuwatunza wanyama.

"Kuna wakati unaweza ukachemsha nyama ya Ng'ombe haichemki au unakula ni ngumu sana, moja ya sababu kubwa kuna wakati unakuta huyo mnyama alinuna sana wakati unamchinja." amesema Edgar.

Aidha Edgar amesema kuwa "kuna sheria ya wanyama inakataza mifugo kama Ng'ombe wasipigwe sana, pia wapumzishwe wanapotembea umbali mrefu".