Thursday , 12th Dec , 2019

ikiwa ni siku mbili tu zimepita tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, kutoa msamaha kwa wafungwa 70 mkoani Njombe, mmoja wa wafungwa hao Musa Msolwa, amekamatwa na Jeshi la Polisi, kwa kuvunja na kuiba kwenye nyumba ya wageni Mjini Makambako.

Mfungwa Mussa Msola akiwa chii ya Ulinzi wa Polisi

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Khamis Issah, amesema mfungwa huyo amedumu nje ya msamaha kwa saa nane tu baada ya hapo akaenda kufanya tukio la uhalifu kwa kuvunja, moja ya nyumba za wageni mkoani Njombe.

"Ni saa nane zimepita mtuhumiwa ambaye aliachiwa kwa msamaha wa Rais,alijikuta anaenda kuvunja gesti ya Nyang'ano, lakini wananchi walimdhibiti." amesema Kamanda Issah.

Akizungumza baada ya kutiwa nguvuni na Jeshi la Polisi, Msolwa amesema kuwa alipitiwa licha ya kuwa aliahidi kubadilika, lakini ameshindwa.