Thursday , 12th Dec , 2019

Baada ya kukamilika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo Desemba 12, 2019, jumla ya timu 16 zimefuzu hatua ya mtoano.

Mchezaji wa Liverpool Roberto Firmino akiwa amebeba kombe la UCL

Mataifa ya England pamoja na Hispania yameendelea kuonesha ubora kwa kutoa vilabu 8 kati ya 16, ambapo kila nchi imetoa timu 4.

Timu zilizofuzu kutoka England ni Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Liverpool, Mabingwa wa EPL Manchester City, Chelsea pamoja na Tottenham.

Kwa upande wa Hispania zilizofuzu ni mabingwa wa Historia wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Real Madrid, Mabingwa wa La Liga Barcelona, Atletico Madrid na Valencia.

Ujerumani na Italia wao wanafuatia kwa kutoa timu nyingi ambapo wametoa timu tatu, ambazo ni Borrusia Dortmund, Bayern Munich na RB Leipzig kwa Ujerumani. Italia ni Juventus, Napoli na Atalanta.
Ufaransa wenyewe wametoa timu mbili ambazo ni PSG na Lyon.

Kwa upande wa timu zilizokwenda kwenye Europa League ni  Bayer Leverkusen, Inter Milan, Ajax Amsterdam, Benfica, Club Brugge, Shakhtar Donetsk, RB Salzbourg na Olympiakos.

Droo ya kupanga hatua hiyo ya mtoano itafanyika mjini Nyon, Switzerland Jumatatu Desemba 16, 2019 saa 7:00 mchana kwa saa za Afrika Mashariki.

Mechi za mtoano zinatarajiwa kuchezwa kati ya 18-19 February na 25-26 February. Mechi za marudiano zitapigwa kati ya 10-11 March na 17-18 March.