Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

DC agawa Mahindi kwa wananchi ili wajisajili NIDA

Monday , 20th Jan , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga Anamringi Macha, amesema kuwa aliamua kugawa Mahindi pamoja na Ndizi mbivu kwa wananchi wake, waliokuwa wamepanga foleni ya kupata namba za utambulisho wa Taifa kutoka NIDA kwa lengo la kuwafundisha uvumilivu na kutokata tamaa katika zoezi hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha

Akizungumza leo Januari 20, 2020, na EATV & EA Radio Digital, DC Macha amesema kuwa lengo lake kuu lilikuwa ni kuwafanya wananchi watulie sehemu moja ili kufanikisha adhma yao ya kupata namba hizo kwa ajili ya kusajili laini zao za simu.

"Niliona nigawe hayo Mahindi na Ndizi kwa sababu, walikuwa na njaa na nilifanya hivyo ili watulie kusubiri huduma na mimi ilikuwa ni kama motivation kwao na kuwafanya wajisikie tuko pamoja na wajifunze kuvumilia, naamini jana kupata kile kidogo kuliwafanya wawe wavumilivu" amesema DC Macha.

Kwa mujibu wa DC Macha amesema ndani ya Wilaya yake, suala la wananchi kujitokeza katika zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya kupata kitambulisho cha Taifa, umeonesha kufana kwa zaidi ya asilimia 80.

Zoezi la usajili wa laini za simu kwa kutumia alama ya Vidole, linahitimishwa leo Januari 20, na kwa wale ambao watakuwa hawajasajili laini zao zitafungwa na kwamba pia zoezi hilo ni endelevu.

HABARI ZAIDI

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90