
Spika wa Bunge, Job Ndugai na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.
Hayo ameyasema leo Januari 31, 2020, katika Mkutano wa 18, Bunge la 11, Kikao cha Nne, wakati wa kipindi cha maswali na majibu juu ya sekta ya elimu na kusema kuwa kitendo alichokifanya Zitto Kabwe si kizuri kwani kinakandamiza haki ya kupata elimu kwa watoto wa wapiga kura wao.
"Waheshimiwa Wabunge wakati mwingine mwenendo wetu haueleweki, mwenzetu Zitto Kabwe atakaporudi labda atafafanulia wenzake, kuandika barua World Bank kwamba nchi yetu ikose fursa ya mkopo ambao lengo lake ni elimu, nadhani ni kwenda mbali mno na sijui katika hilo unafaidika nini kwa sababu kama ni tofauti za kisera hayo ni mambo ya kujadili tu, hili limetugusa na kutukera wengi, baadhi yetu hapa watoto wetu wako feza boys, Marian halafu unablock kwa watoto wa wapiga kura zetu" amesema Spika Ndugai.