Picha ya msanii Gigy Money
Gigy Money ameiambia EATV & EA Radio Digital, kuwa ameshapitia sana mahusiano ambayo mwanaume hana pesa, kilichotokea ni kugombana na kudharauriana.
"Ni kweli nipo kwake kwa ajili ya pesa na anaendelea kunipa, mapenzi bila pesa unakuwa unamsaliti mwanaume wako, ila akiwa anakupa kila kitu kama raha za dunia, kukupa mahitaji na anakupa pesa kwanini usitulie, na kwa mwanaume ambaye hana pesa mimi wa nini sasa hivi" amesema Gigy Money
Aidha Gigy Money ameendelea kusema "Najituma usiku kucha silali nahangaika klabu ili nipate kitu nipeleke nyumbani, kwa hiyo mwanaume ambaye hana pesa tutagombana na kudharauliana tu, bora anipe mawazo ila pesa yake iwe imetumika, nimeshatumika sana kwa mwanaume asiyekuwa na pesa hadi nimechoka waache wenye hela" ameongeza
Gigy Money kwa sasa amerudiana na mpenzi wake huyo ambaye ni raia wa Nigeria Hunchy Huncho, baada ya kutengana kwa kipindi cha muda mfupi.