Monday , 2nd Mar , 2020

EATV & EA Radio Digital imepiga stori na msanii Z Anto ambaye amesimulia kile kilichomkuta mrembo Binti Kiziwi, huko nchini China hadi kupelekea kufungwa miaka 8 kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya.

Pichani Z-Anto akiwa na Binti kiziwi

Z-Anto amesema jambo la kukamatwa kwake lilikuwa baya kwa sababu hakutegemea, hata alivyoambiwa anafungwa miaka 8 akili ilimruka hadi akawa anapewa dawa za usingizi wakati yupo jela.

"Tatizo kubwa ambalo lilimpoteza uraiani alikamatwa na madawa ya kulevya nchini China, akafungwa kwa takribani miaka nane ndiyo amekuja kukanyaga tena Tanzania mwishoni mwa mwaka 2019, japokuwa kila mtu alikuwa anaongea lake na wengine walikuwa wanatamani atoke" ameeleza Z-Anto.

Aidha msanii huyo ameendelea kusema "Alivyokuwa jela nilikuwa nawasiliana naye kwa njia ya simu kila mwezi, alikuwa ananihadithia maisha yake ya kule, mazingira na anavyoendelea" ameongeza.

Pia amesema mrembo huyo Sandra Khan maarufu kama Binti kiziwi, alikuwa mke wake wa ndoa kabisa japokuwa walikuja kuachana kwa makosa binafsi, na miaka mitatu baada ya kuachana kwao ndiyo akasikia amekamatwa.