Picha ya marehemu Baba Kanumba
Kupitia EATV & EA Radio Digital, imempata Happyness Charles ambaye ni mmoja wa watoto wa marehemu Baba Kanumba, akielezea kuhusu sababu ya kifo cha mzee huyo pamoja na ratiba kamili za mazishi ya msiba huo.
"Taratibu za mazishi yenyewe yataanza kesho Jumanne, ambapo tutaaga mwili wa marehemu kuanzia saa 8 mchana kisha kuelekea nyumbani kwao Busega Mwanza, ambapo tutazikia siku ya Jumatano mida ya saa 7 mchana, halafu tutarudi kumalizia msiba nyumbani kwake Shinyanga" ameeleza Happyness Charles.
"Baba ameanza kuumwa kichwa, tumbo na miguu kwa muda mrefu sana, alianza kuugua kabla ya Kanumba hajafariki kwa sababu alikuwa anaumwa polepole, kwahiyo kadri siku zinavyoenda hali inazidi kubadilika ghafla kisha akafariki" ameongeza