Wednesday , 11th Mar , 2020

Jumla ya Shilingi Trilioni 34.88 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika kutokana na mapato ya ndani, mikopo ya nje yenye masharti ya kibiashara, misaada na mikopo nafuu kutoka kwa washirika wa maendeleo, ikiwa ni mapendekezo ya kiwango na ukomo wa bajeti ya mwaka 2020/21,na kuzingatia

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango

mahitaji halisi ya ugharamiaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, ulipaji wa mishahara na deni la Serikali.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango, akiwasilisha mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya kiwango na ukomo wa bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21, jijini Dodoma amesema ukomo wa bajeti hiyo unajumuisha mapato ya ndani ya shilingi Trilioni 24.07 sawa na asilimia 69.0 ya bajeti yote.

Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2020/21, yanatekeleza vipaumbele vilivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21.

Mpango na Bajeti ya mwaka 2020/21 unazingatia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano, chini na uongozi thabiti wa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya kujenga uchumi wa viwanda na kuboresha ustawi wa jamii.