Monday , 25th May , 2020

Alex Gasper “The Rock” Adriko ni mchezaji wa ambaye amejipatia heshima kubwa kwenye timu yake ya Onduparaka FC inayoshiriki Ligi Kuu Uganda.

Alex Gasper “The Rock” Adriko

Jamaa alikuwa na timu hiyo wakati inaanzishwa mwaka 2011 wilaya ya Arua. Ikacheza Ligi ya Wilaya, Ligi ya Mkoa. Ligi daraja la Kwanza na mwaka 2015 ikapanda ligi kuu.

Mpaka sasa anaichezea na wamempa jina la “The Rock” yaani Mwamba.

Amesema faida tatu ambazo amezipata kutokana na kuwa mchezaji wa mpira ni Kukutana na kujuana na watu wengi, Kupata maisha mazuri kutokana na kipato anacholipwa na tatu ni kuepuka kuvuta kutumia mirungi, kuvuta bangi na madawa mengine ya kulevya kutokana na kuwa mbali na marafiki ambao alikuwa nao awali ambao wao kazi yao ni kutumia hivyo vitu.

Alex Gasper akiwa kwenye majukumu yake na Onduparaka FC

Mechi anazozikumbuka sana ni kati ya timu yake ya Onduparaka dhidi ya KCCA kwenye msimu wa kwanza na nyingine ni ya msimu huu dhidi ya mabingwa Vipers.

Anasema ndio mechi ambazo alikuwa kwenye kiwango cha juu zaidi kwenye maisha yake ya soka licha ya kuwa zote alipoteza.

Mechi mbaya zaidi kwake ni dhidi ya Jinja Municipal Council Hippos ambayo ilikuwa kwenye ligi daraja la kwanza. Mwenye anasema hapendi hata kukumbuka.