Wednesday , 27th May , 2020

 Leo Mei 27, 2020, Idris Sultan na mwenzake wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka mawili ikiwemo kumiliki laini ya simu yenye namba 0753-617-621, ambayo imesajiliwa kwa jina la Innocent Maiga.

Msanii wa vichekesho Idris Sultan na mwenzake Innocent Maiga, wakiwa katika Mahakamani.

Idris amepandishwa kizimbani na mwenzake Innocent Maiga, ambaye ameshtakiwa kwa kosa la kutokuripoti mabadiliko ya umiliki wa laini hiyo, ambayo inatumiwa na Idris .

Katika mashtaka hayo wote kwa pamoja wameyakana na kuachiwa kwa dhamana ya kiasi cha shilingi Milioni 15, ambapo keshi hiyo itatajwa tena Juni 9, 2020.

Watuhumiwa wote wawili, wanadaiwa kuyatenda makosa hayo  kati ya Disemba 1, 2019 na Mei 19, 2020, maeneo ya Mbezi Beach katika Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.