Kushoto ni aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe na kulia ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe.
Taarifa hiyo imetolewa kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter wa chama hicho hii leo Juni 30, 2020, ambapo imeandikwa hivi,
"Ndugu yangu Bernard Membe kafukuzwa uanachama wa CCM, ninajua bado anatetea haki yake ya uanachama huko ni hatua sahihi, hata hivyo muda wa kuleta mabadiliko katika nchi umewadia, ninamsihi afanye maamuzi ya kuunganisha nguvu kupitia vyama mbadala" umeeleza ujumbe huo ambao umetolewa na Zitto Kabwe.