Monday , 13th Jul , 2020

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kitendo cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na mchezaji wao Bernard Morrison katika mchezo wa jana wa nusu fainali ya pili ya michuano ya Azam Sports Federation Cup waliolala kwa mabao 4-1 dhidi ya Simba watakichukulia hatua.

Winga machachari wa klabu ya Yanga ,Benard Morrison(Pichani) akiwa na beki kisiki wa wanajangwani hao Kevin Yondan wakiwa mazoezini.

Morrison alifanyiwa mabadiliko dakika ya 68 akaondoka moja kwa moja na hakukaa kwenye benchi kama ilivyo kawaida akionekana kuwa na hasira kwa mabadiliko hayo jambo ambalo uongozi umelitafsiri kuwa ni utovu wa nidhamu.

Afisa Muhamasihaji wa klabu hiyo Antonio Nugaz amesema kila kitu kina utaratibu wake na hatua stahiki zitachukuliwa na zitawekwa wazi.

Kwa upande wa mashabiki wameonyesha kukerwa na mchezaji huo nakusema hata kufungwa kwao kumechangiwa Morriosn ambae alikuwa kama mtalii uwanjani.

Katika mchezo wa jana winga huyo raia wa Ghana alishindwa kuonyesha makeke yake kama ilivyokua katika mechi ya ligi kuu ambayo alifunga bao pekee na la ushindi dhidi ya Simba,huku wengi wakiamini kwamba huenda kwa sasa hayupo tayari kuitumikia klabu hiyo.