Wednesday , 15th Jul , 2020

Ni rasmi kuwa dirisha la usajili la majira ya joto kwa vilabu vya England litakua wazi kwa wiki 10 ambapo litafunguliwa Julai 27 na litafungwa octoba 5 mwaka huu.

Jadon Sancho wa Borussia Dortmund (kulia katika picha) na Kai Harvets wa Bayer 04 Leverkusen (Kushoto),nyota wote hawa wanawaniwa na vilabu vya nchini England.

Kwa kuongezea Bodi ya ligi nchini England imesema kutakua na dirisha la usajili wa wachezaji wa ndani kuanzia octoba 5 hadi 16 .

Wakati wa dirisha hili,vilabu vitaweza kufanya biashara na vilabu vya EFL ama kwa mikopo au usajili wa kudumu.

EFL pia ilisema saini yoyote mpya ya vilabu vyake haiwezi kucheza hadi kuanza kwa msimu wa 2020-21 ingawa bado haijatangazwa tarehe ya kuanza kwa msimu wa 2020-21.