Tuesday , 28th Jul , 2020

Video Vixen na mwanamitandao Zena Haji "Jike Shupa" amesema anagombea Udiwani Kwa Mpangale iliyopo Buza Wilaya ya Temeke kupitia CCM, na sasa hivi anasubiria majibu ya wajumbe ambao wapo kwenye mchakato wa kupiga kura japo anawahofia wasije kumkata.

Video Vixen na Mwanamitandao Jike Shupa

Jike Shupa amesema yupo serious na kugombea Udiwani huo na vipaumbele vyake ni kuwasaidia na kuwaelimisha wanawake kwenye Ujasiriamali wa kujitosheleza pia anaweza kuongoza watu.

"Nasubiria majibu ya Wajumbe wapo kwenye mchakato wa kupiga kura, nipo serious kugombea Udiwani wa Kwa Mpalange iliyopo Buza Temeke kuongoza watu naweza, nawahofia wajumbe maana wao ndiyo wakata umeme, wanachama wa CCM wapo 300 na tunaogombea tupo watano, watu wajiandae kunipokea hata sapoti naipata kutoka kwa watu maarufu na watu wangu wa karibu" amesema Jike Shupa 

Zaidi tazama kwenye video hapa chini.